• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe |
Igunga District Council
Igunga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Utumishi na Utawala
      • Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Uvuvi na Mifugo
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Ugavi
    • Kata
      • Our Wards
  • Vivutio vya Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha Ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Utawala
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
      • UKIMWI
      • Kamati Ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Madiwani
      • Meeting With Chairperson
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkatati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Vituo vya Habari
    • Press Release
    • Video za Shughuli za Ofisi Kitaifa
    • Makitaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi

Maendeleo ya Jamii

Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, ni moja ya Idara mtambuka ambayo lengo lake kuu ni Kusaidia jamii kutafsiri fursa na vikwazo vilivyopo katika mazingira yao na kutumia rasilimali zilizopo kujiletea maendeleo. Utekelezaji wa malengo haya unaongozwa na Sera mbalimbali za Maendeleo ambazo ni pamoja na Sera ya Maendeleo ya Jamii ya 1996, Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya 2000, Sera ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya 2001, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya 2007, Sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi Kiuchumi ya 2004 na Sera ya Taifa ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI ya 2001 na Sheria ya NGOs Namba 24 ya mwaka 2002.

Idara inatekeleza majukumu yake kulingana na dhana ya Maendeleo ya Jamii ambayo inaelezea hatua zinazowezesha watu kutambua uwezo walio nao wa kubaini matatizo na uwezo wao wa kutumia rasilimali zilizopo kujitatulia matatizo hayo, kujipatia na kujiongezea kipato na kujiletea maisha bora zaidi na hivyo kwa ujumla, kujiletea maendeleo.

Katika utekelezaji wake Idara inaratibu mipango ya maendeleo ikiwa ni pamoja na utafiti, mipango na takwimu, masuala ya jinsia, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa (CHF) kwa kushirikiana na Idara ya Afya, Mpango wa Kudhibiti UKIMWI, Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) na uratibu wa asasi zisizokuwa za ki serikali (NGOs, FBOs & CBOs), vikundi vya kiuchumi vinavyotekeleza shughuli zake ndani ya Wilaya ya Igunga na Dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Majukumu ya Idara ya Maendeleo ya Jamii:

  1. Kuiwezesha jamii kushirikisha jamii katika kubaini, kubuni, kupanga, kutekeleza na kufuatilia miradi mbalimbali ya Maendeleo.
  2. Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango/miradi ya Maendeleo.
  3. Kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana na watumishi wa sekta nyingine.
  4. Kuelimisha na kuhamasisha jamii kupambana na VVU na UKIMWI.
  5. Kufanya uchambuzi wa matatizo ya jamii na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ngazi zingine.
  6. Kuvisaidia vikundi maalum (vya ushirika, vikundi vya kijamii, vya kidini, n.k.) kuandaa miradi na kuwaelekeza namna ya kupata mitaji.
  7. Kuelimisha jamii juu ya kutekeleza masuala ya kijinsia na kuratibu shughuli zote za Maendeleo ya Jamii kwa kuzingatia jinsia.
  8. Kuhamasisha jamii kuondokana na mila/desturi zilizopitwa na wakati na kuwa na mtazamo wa kupenda kuleta mabadiliko.
  9. Kuratibu shughuli za mifuko/mikopo ya wanawake.
  10. Kuhamasisha jamii kutumia teknolojia rahisi na sahihi na.
  11. Kuratibu maadhimisho mbalimbali ya Kitaifa na kama vile Siku ya UKIMWI Duniani, Siku ya Mtoto wa Afrika, Mwaka wa kimataifa wa familia, Siku ya wanawake Duniani n.k
  12. Uratibu wa asasi zisizo za kiserikali ndani ya Wilaya

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II October 12, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III October 12, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WATENDAJI WA VIJIJI DARAJA III October 15, 2024
  • TANGAZO LA KAZI July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • MHE. DC. SAUDA MTONDOO AWATAKA MADIWANI KUTEMBEA KIFUA MBELE UTEKELEZAJI ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IGUNGA

    May 16, 2025
  • MHE. DC. SAUNDA MTONDOO APIGA MARUFUKU KUWEKA MAJI, MAWE NA MCHANGA LAINI KWENYE PAMBA

    May 16, 2025
  • DED IGUNGA AWATAKA WENYEVITI WA VIJIJI NA VITONGOJI KUDUMISHA UADILIFU BUSARA NA HEKIMA KUWAHUDUMIA WANANCHI

    May 10, 2025
  • MHE. RC. PAUL MATIKO CHACHA NA MHE. DC. SAUDA MTONDOO WAICHANGAIA IGUNGA UNITED SH. MILIONI 1.8

    April 22, 2025
  • View All

Video

Maadhimisho ya siku Wanawake Kata Simbo ya SIMBO wilayani Igunga.
Video Zaidi

Viungio vya haraka

  • Hotuba
  • Pakua Fomu
  • Zabuni
  • Matangazo ya kibiashara
  • Matukio

Kurasa zinazofanana

  • Watumishi Portal
  • Poralg
  • Public Service Management
  • Tabora Region Website
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Huduma

Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa