Kitengo cha Uchaguzi ni mojawapo ya Vitengo sita (6) vilivyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kikiwa na jukumu la kutekeleza dhana ya Utawala bora na demokrasia kwa wananchi ndani ya Wilaya.
Madhumuni ya kuanzishwa kwa Kitengo hiki ni kumsaidia Mkurugenzi wa Halmashauri kuratibu shughuli zote za uchaguzi kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI).
Ili kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi Kitengo kinaongozwa na Taratibu za uchaguzi zilizoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 74 na 76. Tararatibu hizi pia zimefafanunuliwa kwenye sheria ya Taifa ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985 (sura ya 343). Na Sheria ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Na. 4 ya mwaka 1979 (sura ya 292), Na.7 ya mwaka 1982 (sura ya 287)
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 21, kila raia/mwananchi aliyetimiza umri wa miaka 18 anayo haki ya kushiriki na kutoa maamuzi yoyote yahusuyo uendeshaji wa nchi likiwemo suala la kuchagua viongozi , au kuchaguliwa. Kwa kuwa Tanzania ni nchi ya Kidemokrasia inayofuata mfumo wa vyama vingi, kazi kubwa ya kitengo hiki chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri ni kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Igunga wanapata fursa za kushiriki chaguzi za ngazi zote kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.
Kitengo kina majukuu yafuatayo
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa