Idara ya Elimu Msingi Katika Halmashauri ya wilaya ya Igunga ni moja ya idara ambayo inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Mtaala wa Elimu ya msingi na mtaala wa Elimu ya awali ambayo imeandaliwa kwa kuzingatia viwango vinavyokidhi haja ya kujifunza kwa ufanisi ili kumjengea mwanafunzi umahiri wa elimu ya awali na msingi kwa kuzingatia matakwa ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014. Sera hiyo inaelekeza kuwa elimu msingi ni ya lazima kwa kila mtoto wa Tanzania.
Sekta ya elimu na mafunzo, kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 na mpango wa muda mrefu wa maendeleo ya Taifa 2011/12 hadi 2014/25, inatarajiwa kuleta maendeleo ya haraka ya rasilimali watu kwa kutayarisha idadi ya kutosha ya Watanzania walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili kulifanya Taifa lipate maendeleo na kuwa lenye uchumi wa kati na shindani ifikapo 2025.
Katika Wilaya ya Igunga huduma ya utoaji elimu ya Awali na Msingi inafanyika kwa ushirikiano kati ya Halmashauri na wadau mbalimbali wa maendeleo waliopo katika Wilaya. Halmashauri ina jumla ya shule za Msingi 137 zilizosajiliwa, ambapo Shule 133 ziko chini ya umiliki wa serikali 1 zinamilikiwa na watu binafsi na 3 zinamilikiwa na taasisi za dini. Aidha usimamizi wa shule uko chini ya afisa Elimu Msingi katika ngazi ya Wilaya na Afisa Elimu Kata kwa ngazi ya kata.
Idara ya Elimu Msingi inaundwa na vitengo vitatu katika kutekeleza majukumu yake. Vitengo hivi ni kama ifuatavyo:-
MAJUKUMU YA IDARA YA ELIMU MSINGI
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa