Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ina vituo 66 vya kutolea huduma za afya kwa wananchi wake, vituo hivi vinaanzia ngazi ya Wilaya ( Hospitali ya Wilaya) hadi Kijiji (Zahanati). Huduma zimekuwa zinatolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali waliopo ndani ya Wilaya ambazo zimejikita katika sehemu kubwa ya Afya tiba na kinga. Vituo hivyo ni kama ifuatavyo: tunazo Hospitali 2, moja iko chini ya umiliki wa Serikali na nyingine ni Hospitali ya rufaa ya Nkinga ambayo inayomilikiwa na shirika la dini (FPCT), tunavyo vituo vya afya vitano (5) ambapo kituo kimoja cha afya kinamilikiwa na shirika la dini na 4 vinamilikiwa na serikali. Pia katika Wilaya kuna jumla ya zahanati 59, ambapo zahanati 53 ni za serikali na zahanati mbili (2) ziko chini ya umiliki wa mashirika ya dini na zahanati tatu (3) zinamilikiwa na watu binafsi na moja (1) inamilikiwa na Jumuiya ya wazazi. Aidha utoaji wa huduma za afya unatekelezwa chini ya usimamizi wa Mganga Mkuu wa Wilaya kwa kuzingatia miongozo na taratibu mbalimbali zinazotolewa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto.
Majukumu ya Idara:
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa