Fursa za kibiashara katika sekta ya mifugo
Utangulizi
Sekta ya mifugo ina umuhimu mkubwa katika kujenga uchumi imara ambao utapelekea kuleta usawa baina ya watanzania kwa kuwaongezea kipato na kuwapatia fursa za ajira. Sekta ya mifugo in umuhimu mkubwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania kwa kuimarisha usalama wa chakula, kuchangia katika uchumi wa taifa, kuongezeka kwa kipato na kutengeneza fursa za ajira kwa jamii za vijijini na mijini. Mafanikio ya sekta ya mifugo yatatokana na kuwajengea wadau wa sekta ya mifugo kuendesha sekta kisasa na kibiashara kwa kufuga mifugo inayokuwa haraka, yenye uzalishaji mkubwa hivyo kupelekea upatikanaji wa mifugo na mazao ya mifugo bora.
Wilaya ya Igunga ni miongoni mwa Wilaya zenye Mifugo mingi katika Mkoa wa Tabora ikiwa km za mraba 513 zinafaa kwa malisho ya mifugo na mifugo 1,841,719 kwa mchanganuo ufuatao katika jedwali na.
Jedwali Na. 1 Takwimu za mifugo wilayani Igunga
Aina ya Mifugo
|
Idadi |
|
Asili |
Kisasa |
|
Ng’ombe
|
685,416 |
1,876 |
Mbuzi
|
364,252 |
178 |
Kondoo
|
195,024 |
0 |
Kuku
|
552,615 |
4081 |
Bata
|
5,181 |
0 |
Nguruwe
|
9,200 |
17 |
Punda
|
11,055 |
0 |
Mbwa
|
9,182 |
0 |
Paka
|
3,642 |
0 |
Jumla
|
1,835,567 |
6,152 |
Fursa katika sekta ya mifugo
Zipo fursa nyingi zinazoweza kuongeza mchango wa mifugo katika uchumi na uhakika wa chakula kuanzia ngazi ya kaya,Halmashauri na Taifa ikiwa fursa hizo zitatumika ipasavyo,fursa hizo ni pamoja na:.
Idadi kubwa ya mifugo hii ni ya asili, hata hivyo pamekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya ng’ombe wa maziwa kutoka ng’ombe 70 mwaka 2005 hadi ng’ombe 1876 mwaka 2017, pia uzito wa ng’ombe kutoka kilo 200 mwaka 2005 hadi kilo 500 mwaka 2017.
Ndama bora aliyetokana na upandishaji kwa kutumia dume bora.
Masoko ya uhakika ya mifugo na mazao yake,mji wa Igunga upo katika barabara kuu ya Dar-es Salaam,Mwanza,Tabora,Kahama,Kigali,Bunjumbura,Goma na Kampala,hii ni fursa muhimu kwa mifugo na mazao yake. Mji wa Igunga una huduma zote muhimu za kijamii ( afya,usafiri,malazi,mahoteli safi, umeme) na kifedha (NMB CRDB, ,Mpesa ,Tigo Pesa na Airtel Money, Halopesa)
Upatikanaji wa watu wanaoweza kufunzwa na gharama nafuu za nguvu kazi.
Halmashauri ina wataalam katika sekta mbalimbali k.v mifugo,kilimo,ardhi,mazingira, maendeleo ya jamii,ushirika utawala, maji na fedha wanaounda timu kabambe ya wawezeshaji wa wilaya.
Halmashauri imetenga ekari 157.69 kwa ajili ya viwanda vidogo na ekari 84 kwa ajili ya viwanda vikubwa, maeneo haya yanaweza kutumika kwa ajili ya viwanda vya ngozi, maziwa ,nyama na vyakula vya mifugo.
Vivutio vya uwekezaji katika sekta ya mifugo
Uwekezaji unaweza kufanyika katika maeneo yafuatayo:-
Kuanzisha vituo vya kunenepesha ng’ombe (Mnada wa Igunga, Mnada wa Iborogero na Shamba la Bulyashiri).
Viwanda vya usindikaji wa nyama ( kuchinja kwa ajili kupeleka kwenye viwanda vikubwa).
Viwanda vya usindikaji wa maziwa ( kituo cha kukusanya na kupooza maziwa kwa ajili ya viwanda).
Viwanda vya usindikaji wa ngozi
Kuanzisha vituo vya kukusanya,kukagua, kuchinja na kuuza kuku
uzalishaji wa vyakula vya mifugo
Uwekezaji kwenye masoko ya mifugo (mabucha,majiko,meza n.k)
Takwimu za ongezeko la miundombinu na uzalishaji wa mifugo
|
Sekta ya mifugo
|
2014/2015
|
2017/2018
|
Asilimia ya ongezeko
|
|
1
|
Banda la ngozi
|
1
|
2
|
50
|
|
2
|
Ng’ombe bora wa maziwa
|
1123
|
1876
|
67
|
|
3
|
Majosho
|
19
|
20
|
5
|
|
4
|
Madume bora ya ng’ombe
|
262
|
603
|
130
|
|
5
|
Mashamba darasa
|
3
|
7
|
133
|
|
6
|
Vikundi vya wafugaji
|
21
|
62
|
195
|
|
8
|
Minada ya mifugo
|
3
|
4
|
33
|
|
9
|
Uzalishaji wa mazao ya mifugo
|
Nyama (tani)
|
449.68
|
642.4 |
30
|
Maziwa (lita)
|
61,687,427
|
65,774,080 |
6.6
|
||
Mayai
|
4,752,798
|
6,789,712 |
30
|
Matukio ya magonjwa yanayoenezwa na kupe (Ndigana kali na baridi,kukojoa damu na majimoyo) yamepungua kutoka asilimia 70% mwaka 2010 hadi asilimia 30%.mwaka 2017.
Uzito wa ng’ombe wa miaka 3-5 kutoka kilo 150-200 hadi kilo 350-500 kwa ng’ombe
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa