MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Mhe. Shabani Hemed amewataka vijana waliopewa Pawatila za Halmashauri kuziendesha kwa uaminifu jambo ambalo linatafsiri utu na kazi vinavyotekelezwa na Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa vijana nchini.
Mhe. Hemed ametoa wito huo Jumanne Februari 10, 2025 katika viwanja vya Halmashauri hiyo wakati akikabidhi Pawatila Sita zilizoletwa na serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa lengo la kuendelea kutuoa huduma kwa wananchi.
"Nendeni mkawe waadilifu kwa sababu sisi Halmashauri hatufanyi biashara ispokua kazi yetu ni kuhakikisha tunawahudumia wananchi, hivyo nilazima muwe na utu wa kutunza hizi zana," amesema na kuongeza kuwa:
"kafanyieni kazi ziwasaidie nyinyi na jamii inayowazunguka na kwa jambo hili tunamshukuru Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea hizi zana."
Katika hatua nyingine, Mhe. Hemed amewahimiza vijana waje wakope fedha kwa lengo la kuwawezesha kuendesha mashamba yao wakati wakiendesha Pawatila hizo.
"Ndugu zangu vijana serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeleta mikopo hii kwa lengo la kuwawezesha vijana, hivyo msisubiri muda ukaisha mkaanza kulalamika sio jambo jema, njooni mkope mkalime kwa tija," ametoa wito.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bi. Selwa Hamid amewasihi waendeshaji hao kuwa waaminifu na kutofanya ubadhirifu au upendeleo katika kutoka huduma.
"Katendeni haki na mkatoe huduma bora na kwa bidii kwa sababu Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametuelekeza sisi watumishi kupeleka tabasamu kwa wanannchi, hivyo tutoe huduma vizuri," amesema.
Naye Mwenyeketi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Igunga, Fabian Lushindika amewapongeza vijana ambao wamekabidhiwa Pawatila hizo huku akiwaasa kuvitendea haki.
"Ninategemea ufanisi wa kazi utakua mzuri, hivyo mkatende haki kwa lengo la kuhakikisha matokeo ya kazi zenu yaonekane kwa wananchi," amesema.
============================/


Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa