Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Ndugu Revocatus L.K. Kuuli, amewapongeza Shirika la Care Tanzania kupitia Mradi wa TAMANI (Tabora Maternal and New born Initiatives), kwa huduma waliyoitoa ya vifaa tiba pamoja na vitanda kwa Halmashuri ya Wilaya ya Igunga, katika kikao cha kamati ya Fedha kilichoketi jana tarehe 08.01.2019, katika ukumbi wa Halmashuri ya Wilaya ya Igunga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mheshimiwa Peter Onesmo Maloda, aliendelea kuwasisitiza ushirikiano na taasisi zinazotuzunguka kwani zinasaidia halmashauri yetu katika nyanja mbalimbali.
“Halmashauri ya Wilaya ya Igunga tunayo furaha kubwa kwa heshima iliyoonyeshwa na Care Tanzania, chini ya mradi wa TAMANI (Tabora Maternal and New born Initiatives). Bi.Catherine Mathias ambaye ni mwakilishi hapa Igunga alitukabidhi vifaa vyenye thamani ya Tsh.88, 535,600.00, leo kwa kutambua umuhimu wao tunamtunuku cheti cha kutambua mchango wa Care Tanzania kwa halmashauri yetu hii” aliongenza Bwana Revocatus L.K.Kuuli Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Igunga.
Naye Mwakilishi wa Care International Tanzania Wilaya ya Igunga Bi.Catherine aliwashukuru wajumbe wa kamati ya Fedha kwa ukaribisho wao, akaomba kufanya nao kazi bega kwa bega ili kuendelea kuimalisha utoaji wa huduma za Afya Wilayani Igunga.
Care International Tanzania chini ya Mradi wake wa TAMANI (Tabora Maternal and New born Initiatives), Shirika la Care kupitia mradi wake wa TAMANI umelenga kuchangia jitihada za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, kwa kuboresha upatikanaji wa hiduma bora za afya kwa wajawazito, watoto, wanawake na familia zao.Utekelezaji wa mradi unafanyika katika zahanati 46, kata 33 na vijiji 64 wilayani Igunga.
Mkurugrenzi amemaliza kwa kuwaomba Care International Tanzania kuendelea kusaidia pale watakapo pata vifaa vingine ili kuendelea kuboresha huduma ya Afya Wilayani Igunga kwani Halmashauri peke yake na Serikali haiwezi kutimiliza mahitaji yote kwa wananchi wa Wilaya ya Igunga katika utoaji wa huduma za afya.
Imetolewa na
Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa