Bw;Simon P. Malando,Afisa Tarafa ya Igunga ametoa maelekezo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amewataka Watendaji wa Kata kuhakikisha wanashirikiana na Wananchi kuhakikisha Watoto wanapata chakula shuleni,Watendaji ambao wamefikia asilimia 83 ya utoaji chakula shuleni katika Kata zao,walipata nafasi ya kueleza mbinu walizotumia hadi kufanikiwa,mbinu pekee inayoleta mafanikio ni kufanya vikao na wananchi na kukubaliana kiasi cha kuchangia,pia Mchangiaji anaruhusiwa kutoa kidogokidogo kutokana na kipato hadi amalize kiwango kilichokubaliwa kwenyekikao.(Walisema Watendaji wa Kata)
Mikakati na maadhimio iliwekwa kuwa kila Kata viongozi wa Chama na Serikali waseme kauli moja kwa wananchi juu ya uchangiaji chakula cha watoto Shuleni.
Divisheni za Halmashauri zinzojishughulisha na mikakati ya kuhakikisha Jamii inakuwa na Lishe bora walitoa taarifa za mafanikio ya utendaji kazi katika robo ya kwanza 2023/2024,Halmashauri ya Igunga inaelewa umuhimi wa Lishe bora katika kujenga Jamii imara yenye kujenga Taifa Bora.Pia uongozi wa Halmashauri unaheshimu na kusimamia Mikataba ya Lishe iliowekwa baina ya viongozi,Mhe SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunamshukuru kwa kulitilia mkazo mkubwa suala la Lishe katika Jamii zetu ili ziweze kuwa na afya njema na kutekeleza na kujenga familia zinyeafya imara.Halmashauri imejiwekea mikakati kupitia Divisheni ya kilimo,mifugo na Uvuvi ya kuhakikisha jamii inalima vyakula vya aina tofautitofauti ili kuwa na chakula bora.
LISHE DIVISHENI YA KILIMO,
MIFUGO NA UVUVI.
Katika msimu wa kilimo wa 2023/2024 Wilaya ya Igunga imelenga kulima hekta 83,809 za mazao ya nafaka na mizizi zinazotarajiwa kuzalisha tani 289,315 ili kuhakikisha upatikanaji wa Wanga, hekta 15,724 za mazao ya mikunde zinazotarajiwa kuzalisha tani 15,724 ili kuhakikisha upatikanaji wa Protini na hekta 1,855 za mazao ya bustani ambazo zinatarajiwa kuzalisha jumla ya tani 6,647.9 ili kuhakikisha upatikanaji wa Vitamini
Hadi kufikia Juni 2023 Jumla ya Hekta 69,312 za mazao ya nafaka na mizizi zilikuwa zimelimwa na kuzalisha Jumla ya Tani 134,902 za mazao ya nafaka na mizizi. Kwa upande wa zao la mikunde Jumla ya Ha 13,520 zilikuwa zimelimwa na kuzalisha Jumla ya Tani 8,091.3 za zao la mikunde.
Hivyo ukilinganisha na mahitaji ya Tani 129,586.9 za nafaka zinazohitajika kwa mwaka kutosheleza watu 546,204 waliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Wilaya ilikadiriwa kuwa na ziada ya takribani Tani 5,315.1 za nafaka ghalani zilizozalishwa kwa msimu wa kilimo 2022/2023.
Jumla ya wakulima 1,328 wamepatiwa elimu ya kilimo cha Mbogamboga ili kuhakikisha upatikanaji wa vitamini itokanayo na mazao ya bustani. Kati ya hao wakulima 1,184 wamepata elimu kupitia siku ya wakulima Nanenane na wakulima 144 wamepata elimu kupitia njia mbalimbali za huduma za ugani.
KITENGO CHA LISHE
Jumla ya maeneo 93, maduka 74 ya vyakula,mashine 12 za kusaga na kukoboa nafaka na sehemu 6 za usindikaji wa mafuta yalikaguliwa.Watoto 14 (Me 8 na Ke 6) walipata matibabu ya utapiamlo mkali.Kata zote 35 na vituo vya afya 65 vya Wilaya ya Igunga zilikusanywa na zinaendelea kuingizwa kwenye mfumo wa taarifa wa IMES. Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yalifanyika na elimu ya lishe juu ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama yalitolewa kwa wananchi wa kata ya Mwanzugi.
Usimamizi katika vituo vyote ulifanyika katika vituo 4 vya kulea watoto wadogo mchana.Tulifanikiwa kufanya jiko darasa katika vijijini 19 sawa na asilimia 95
LISHE – ELIMU MSINGI,
Shule 139 kati ya shule 139 za serikali zilitoa uji/chakula cha mchana kwa wanafunzi shuleni,Pamoja na halingumu ya mavuno msimu iliyopita lakini wazazi baadhi wameahidi kutoa chakula shuleni ili watoto wapate hata uji wa asubuhi.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa