WAHESHIMIWA Madiwani kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Bi. Selwa Abdalla Hamid wakiwemo baadhi ya Wataalamu wa Halmashauri hiyo wamefanya ziara ya kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Viongozi hao wamefanya ziara hiyo Jumanne Disemba 17, 2024 jijini Dodoma na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu Bunge.
Katika ziara hiyo walikutana na Afisa Mwandamizi anayefanya kazi katika Bunge hilo, Patson Sobha ambae aliwaeleimisha namna ambavyo Bunge linafanya shughuli zake.
=====//////======
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa