• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe |
Igunga District Council
Igunga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Utumishi na Utawala
      • Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Uvuvi na Mifugo
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Ugavi
    • Kata
      • Our Wards
  • Vivutio vya Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha Ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Utawala
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
      • UKIMWI
      • Kamati Ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Madiwani
      • Meeting With Chairperson
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkatati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Vituo vya Habari
    • Press Release
    • Video za Shughuli za Ofisi Kitaifa
    • Makitaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi

MIKAKATI YA KUKABILIANA NA ATHARI ZINAZOWEZA KUJITOKEZA KUTOKANA NA MVUA ZA ELNINO ZINAZOTARAJIWA MSIMU HUU WA 2023/2024.

Tarehe iliyowekwa: November 9th, 2023

Kamati ya Maafa Wilaya ya Igunga imekaa na kubainiasha Athari zinazoweza kujitokeza kutokana na Mvua za Elnino zinazotajiwa Msimu wa Mwaka 2023/2023,Kikao kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga 9/11/2023,kikiongozwa na Mwenyekiti wa Maafa ambaye ni Mhe;Sauda Mtondoo Mkuu wa Wilaya ya Igunga.Athari zilibainishwa na kuweka Mikakati ya kukabiliana na Athari hizo kama zinavyoonekana katika Jedwari hapo chini.

MIKAKATI YA KUKABILIANA NA ATHARI ZINAZOWEZA KUJITOKEZA KUTOKANA NA MVUA ZA ELNINO ZINAZOTARAJIWA MSIMU HUU WA 2023/2024.

NA:
 ATHARI ZINAZOTARAJIWA
MIKAKATI YA KUKABILIANA NA ATAARI
1 Mafuriko kutokana na mvua nyingi
  • Wataalam wa  wa sekta mbalimbali  kufuatilia kutafsiri na kusambaza kwa wananchi taarifa za hali ya hewa za mara kwa mara ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.
  • Wananchi  wanashauriwa kuhama maeneo ya mabonde ili kuepuka  athari zitakazotokana na mvua nyingi.
  • Wavuvi wanashauriwa kuondoa nyumba na makambi yaliyopo kwenye    bonde la Wembele.
  • Kuwasiliana na shirika la msalaba mwekundu juu ya kupata usaidizi pindi athari zitakapojitokeza.
2 Kuharibika kwa miundombinu ya barabara, madaraja, umeme na maji
  • Kuandaa bajeti ya dharura kukabiliana na athari hizi
3 Kusimama au kupungua kasi kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali kutokana na kuharibika kwa miundombinu ya barabara  na kupelekea kutofikishwa kwa mahitaji ya ujenzi
  • Halmashauri kuwasiliana na sekta/taasisi husika ili kuzishauri sekta husika kutenga bajeti ya dharura kukabiliana na athari zitakazojitokeza.
4 Ongezeko la utoro kwa wanafunzi kutokana na kuharibika kwa miundombinu ya barabara kuelekea shuleni
  • Halmashauri kuwasiliana na sekta/taasisi husika ili kuzishauri sekta husika kutenga bajeti ya dharura kukabiliana na athari zitakazojitokeza.
5 Kuharibika kwa makazi mfano kubomoka kwa nyumba kunakoweza kusababishwa na maji yaliyotuama kwa muda mrefu katika makazi na kuezuliwa kwa majengo kunakoweza kusababishwa na pepo kali zinazoweza kuambatana na mvua nyingi.
  • Kuwasiliana shirika la msalaba mwekundu juu ya kupata usaidizi pindi athari zitakapojitokeza.
  • Kutenga  maeneo/majengo ya taasisi yatakayotumika kuhifadhi wahanga. 
6 Kuharibika kwa mashambaa kutokana na mmomonyoko wa ardhi unaoweza kusababishwa na mafuriko.
  • Wakulima na wadau wengine wahamasishwe kuboresha mifereji ya matupio ya maji kwenye maeneo ya kilimo ili kuwezesha maeneo yatakayopata mvua za juu ya wastani yaweze kutumika katika kilimo.
7 Upungufu wa chakula unaoweza kutokea kutokana na mazao kusombwa na mafuriko au mazao hayo kutofanya vizuri kwa maji kutuama kwa muda mrefu shambani.
  • Wakulima kutumia mvua hizo kupanda mazao yanayohimili viwango vikubwa vya unyevu ardhini kama vile mpunga na kuzingatia kanuni bora za kilimo ikiwemo kupanda kwa wakati.
  • Wananchi wahamasishwe kuandaa na kuhifadhi chakula cha ziada kinachoweza kutumika kipindi cha dharura.
8 Ongezeko la mlipuko wa magonjwa mfano kipindupindu, kuhara, malaria na homa ya matumbo
  • Kuandaa na kuweka tayari vituo vya kutolea huduma za afya ili kukabiliana na mlipuko wa magonjwa
  • Elimu ya afya kuendelea kutolewa kwa wananchi kuhusu usafi na matumizi ya vyoo bora
9 Mlundikano wa taka kutokana na taka hizo kusombwa na maji toka maeneo mengine
  • Kusimamia usafishaji na uzibuaji wa mitaro ili kuruhusu maji kutotuama
  • Kuwasiliana na TARURA ili kuboresha miundombinu ya mitaro ya barabara katika maeneo yanayotarajiwa kuathirika.
10 Kupungua kwa upatikanaji wa maiji safi na salama kutokana na vyanzo vya maji kuchafuliwa na tope linalotokana na mafuriko
  • Wananchi  kutengeneza na kukarabati miundumbinu ya kuhifadhi maji ambayo yatatumika katika kipindi cha msimu wa kiangazi.
11 Kuongezeka kwa gharama za kusafisha maji kutokana na maji kuchafuliwa na tope.
  • Kuwasiliana na  RUWASA na IGUWASA ili kuchukua tahadhari juu ya athari hizi
12 Kung’oka na kuanguka kwa miti kutokana na mmomonyoko wa udongo   Upepo mkali unaoweza kuambatana na mvua kubwa.
  • Kutoa elimu kwa wananchi kuepuka kuwa karibu na miti mikubwa hususani kipindi cha mvua na upepo mkali

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II October 12, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III October 12, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WATENDAJI WA VIJIJI DARAJA III October 15, 2024
  • TANGAZO LA KAZI July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • MHE. RC. PAUL MATIKO CHACHA NA MHE. DC. SAUDA MTONDOO WAICHANGAIA IGUNGA UNITED SH. MILIONI 1.8

    April 22, 2025
  • MHE. DC. SAUNDA MTONDOO KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WATAKAOWEKA UCHAFU KWENYE PAMBA

    April 22, 2025
  • WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAHAKIKISHIA WANANCHI KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZOTE KARIBU YAO IGUNGA

    March 12, 2025
  • WANAWAKE WAKUMBUSHWA UMUHIMU WAO DUNIANI

    March 09, 2025
  • View All

Video

Maadhimisho ya siku Wanawake Kata Simbo ya SIMBO wilayani Igunga.
Video Zaidi

Viungio vya haraka

  • Hotuba
  • Pakua Fomu
  • Zabuni
  • Matangazo ya kibiashara
  • Matukio

Kurasa zinazofanana

  • Watumishi Portal
  • Poralg
  • Public Service Management
  • Tabora Region Website
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Huduma

Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa