Serikali imewaagiza Watendaji wa Halmashauri nchini kuhakikisha wana kusanya mapato kwa kuzingatia sheria,taratibu na kanuni na kwamba fedha zote ziwekwe benki ndani ya saa 24.
Kauli hiyo imetolewa wilayani Igunga na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa (OR TAMISEMI) Ummy Mwalimu akizunguma na Madiwani na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
Waziri Ummy alisema Halmashauri ya Wilaya ya Igunga fedha inaonekana inapelekwa benki lakini mapato yanayoonekana ni kidogo kwa kuwa mifumo ya kukusanyia mapayo kwa njia ya kielektroniki haitumiki ipasavyo.
Aliongeza fedha nyingi zitumika kabla hazijaingia benki kutokana na kisingizio cha kuharibika kwa mashine za kukusanyia mapato au kutokuwepo kwa mapato kwenye baadhi ya maeneo.
“Watendaji zingatieni maelekezo ya Serikali, ya kukusanya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kutumia mifumo ya kielektroniki, kwa kuhakikisha mapato ya ndani yaliyokusanywa yanawasilishwa benki ndani ya saa 24 kabla hayajatumika” alisisitiza
Aliwataka Madiwani na Kamatiya fedha kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato ili Halmashauri ya Wilaya ya Igunga iweze kuwa na fedha nyingi za kupeleka na kuboresha huduma mbalimbali kwa wananchi
Aidha, Waziri Ummy aliwatataka Viongozina Watendaji wote kudumisha ushirikiano ili waweze kutimiza wajibu wao kusimamia mapato na matumizi ya fedha za Halmashauri hiyo kuwa itasaidia kuweka sawa mahesabu ya fedha vizuri na kupunguza hoja za ukaguzi.
Katika hatua nyingine Ummy amewatakawazazi wenye watoto waliopata ufaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tanokwenye shule za Serikali hapa nchini ambao wanakusudia kuwapeleka katika Shulebinafsi kuhakikisha wanatoa taarifa mapema ili nafasi hizo wapewe wanafunziambao wamefaulu lakini hawakupata nafasi za kujiunga na shule za Serikali.
Alisema jumla ya wanafunzi 86,896wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano lakini wanafunzi wapatao 3,800wamekosa nafasi ya kujiunga na kidato cha tano kutokana na uhaba wa nafasihizo.
Ummy aliongeza itakuwa vema kama wazazi na walezi wa wanafunzi waliopata nafasi kwenye shule za Serikali lakini hawataki kuwapeleka watoto wao huko watoe taarifa ili wale waliokosa nafasi wapate kuendelea na masomo kidato cha tano.
Aidha, Waziri Ummy aliahidi kupelekafedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya sekondari Ziba ili kuondoa kero inayowakabili wanafunzi wa shule hiyo.
Kwa upande wa Mbunge wa jimbo la Manonga wilayani Igunga Seif Gulamali alisema jumla ya shule 15 za msingi na 13 za sekondari zimepatiwa fedha na Serikali kiasi cha shilingi milioni 807 ili kujenga miundombinu mbalimbali.
Alisema mapema mwaka ujao wa fedhawanatarajia kupokea shilingi milioni 700 kwa ajili ya kujenga shule yawasichana ambayo itakuwa imekamilika kwenye miundombinu yote.
Gulamali alitoa shukurani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wananchi kote nchini.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa